Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 118

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2Israeli na aseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
3Nyumba ya Haruni na iseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
4Wafuasi waaminifu wa Yahwe na waseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
5Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe; Yahwe alinijibu na kuniweka huru.
6Yahwe yuko pamoja nami; sitaogopa; mwanadamu atanifanya nini? Yahwe yuko upande wangu kama msaidizi;
7nitawatazama kwa ushindi wale walio nichukia.
8Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu.
9Ni bora kukimbilia katika Yahwe kuliko kuamini katika wakuu.
10Mataifa yote walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
11Walinizunguka; naam, walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
12Walinizunguka kama nyuki; walitoweka haraka kama moto kati ya miiba; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
13Walinishambulia ili waniangushe, lakini Yahwe alinisaidia.
14Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu, na ndiye anaye niokoa.
15Kelele za ushindi zimesikika katika maskani ya wenye haki; mkono wa kuume wa Mungu umeshinda.
16Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda.
17Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe.
18Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife.

19Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe.
20Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo.
21Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu.
22Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi.
23Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu.
24Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.
25Tafadhali, Yahwe, utupe ushindi! Tafadhali, Yahwe, utupe mafanikio!
26Amebarikiwa yule ajaye katika jina la Yahwe; tunakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe.
27Yahwe ni Mungu, na ametupa sisi nuru; ifungeni dhabihu kwa kamba pembeni mwa madhabahu.
28Wewe ni Mungu wangu, nami nitakushukuru; wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe.
29Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema; kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.