Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 91

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yeye aishiye katika makazi ya Aliye Juu atakaa katika uvuli wa mwenyezi.
2Nami nitasema kuhusu Yahwe, “Yeye ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye niaamini katika yeye.”
3Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti.
4Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
5Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
6wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
7Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
8Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
9Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
10Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
11Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.
12Nao watakuinua juu kwa mikono yao ili usiweze kujigonga mguu wako kwenye jiwe.
13Utawaangamiza simba na nyoka chini ya miguu yako; utawakanyaga wana-simba na nyoka.
14Kwa sababu amejitoa kwangu, nitamuokoa. Nitamlinda kwa sababu yeye ni mwaminifu kwangu.
15Aniitapo, nitamjibu. Katika shida nitakuwa naye; nitampatia ushindi na nitamuheshimu.
16Nitamtosheleza kwa maisha malefu na kumuonesha wokovu wangu.