1Unilinde, Mungu, kwa kuwa nakimbilia kwako kwa ajili ya usalama.
2Nami ninasema kwa Yahwe, “Wewe ni Bwana wangu; wema wangu ni bure pasipo wewe.
3Kama kwa watakatifu walioko duniani, ndio walio bora; furaha yangu yote iko kwao.
4Taabu yao itaongezeka, wale watafutao miungu mingine. Sitamimina sadaka ya damu kwa miungu yao. Wala kuyainua majina yao kwa midomo yao.
5Yahwe, wewe ni sehemu ya chaguo langu na kikombe changu. Unaishikilia kesho yangu.
6Mistari iliyo pimwa imelelazwa mahari pa kufurahisha kwa ajili yangu; hakika urithi ufurahishao ni wangu.
7Nitakubariki Yahwe, wewe unishauliye; hata wakati wa usiku akili zangu za nielekeza.
8Nimemuweka Yahwe mbele yangu kila wakati, ili nisitikisike kutoka mkono wake wa kuume.
9Kwa hiyo moyo wangu unafuraha, utukufu wangu washangilia. Hakika nitaishi katika usalama.
10Kwa kuwa hautaiacha roho yangu kuzimuni. Wewe hautamuacha mwaminifu wako kuliona shimo.
11Wewe hunifundisha njia ya maisha; furaha tele inakaa katika uwepo wako; furaha inakaa katika mkono wako wa kuume milele!”