Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 95

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Oh njoni, tumwimbie Yahwe; na tumwimbie kwa shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2Tuingie uweponi mwake kwa shukrani; tumwimbie yeye kwa zaburi ya sifa.
3Kwa maana Yahwe ni Mungu mkuu na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake zimo bonde za dunia; navyo vilele vya milima ni vyake.
5Bahari ni yake, maana aliiumba, na mikono yake ilitengeneza nchi kavu.
6Oh njoni, tumwabudu na tupige magoti; tupige magoti mbele za Yahwe, muumbaji wetu:
7Kwa maana yeye ni Mungu wetu, na sisi tu watu wa malisho yake na kondoo wa mkono wake. Ni heri leo mngesikia sauti yake!
8Msiifanye migumu mioyo yenu, kama vile huko Meriba, au kama ile siku ya Masa jangwani,
9ambako baba zenu walinijaribu na kunipima, japo walikuwa wameyaona matendo yangu.
10Kwa miaka arobaini nilikasirishwa na kizazi hicho na kusema, 'Hawa ni watu ambao mioyo yao imepotoka; hawazijui njia zangu.'
11Hivyo katika hasira yangu niliapa kwamba wasingeingia kamwe mahali pa pumziko.”