1Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe.
2Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma.
3Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama?
4Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa.
5Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia.
6Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi.
7Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe.
8Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.