1Ee Mungu, moyo wangu u thabiti; nitaimba, naam, nitaimba sifa pia kwa moyo mkuu.
2Amka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
3Nitakushukuru wewe, Yahwe, kati ya watu; nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
4Kwa maana uaminifu wa agano lako ni mkuu juu ya mbingu; na uaminifu wako wafika mawinguni.
5Ee Mungu, uinuliwe, juu ya mbingu, na utukufu wako utukuke juu ya nchi.
6Ili kwamba wale uwapendao waokolewe, utuokoe sisi kwa mkono wako wa kuume na unijibu.
7Mungu ameongea katika utakatifu wake; “Nitashangilia; nitaigawanya Shekemu na nitalipima bonde la Sukothi.
8Gileadi ni yangu, na manase ni yangu; Ephraimu ni nguvu ya kichwa changu; Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.
9Moabu ni bakuli langu la kunawia; nitatupa kiatu changu juu ya Edomu; nitapaza sauti katika ushindi kwa ajili ya Filisti.
10Ni nani atakaye nipeleka kwenye mji imara? Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?”
11Ee Mungu, sio wewe uliyetukataa? Hauendi vitani na jeshi letu.
12Utupe msaada dhidi ya adui yetu, maana msaada wa wanadamu ni bure.
13Tutashinda kwa msaada wa Mungu; atawakanyaga kwa adui zetu.