1Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”
2Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako.
3Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande.
4Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme.
6Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi.
7Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu.