Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu, uniletee haki, na unitetee dhidi ya taifa lisilo la kimungu.
2Kwa kuwa wewe ni Mungu wa nguvu zangu. Kwa nini umenikataa? Kwa nini ninaenenda katika maombolezo kwa sababu ya ukandamizaji wa adui yangu?
3Oh, tuma nuru yako na kweli yako ziniongoze. Ziniletee mlima wako mtakatifu na makao yako.
4Kisha nitakwenda madhabahuni mwa Mungu, kwa Mungu wangu aliye furaha yangu kuu. Nami nitakusifu wewe kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu.
5Roho yangu, kwa nini umeinama? Kwa nini unahuzuni ndani yangu? Kwa kuwa nitamsifu tena yeye ambaye ni wokovu wangu na Mungu wangu.