Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 100

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote.
2Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha.
3Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.
5Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.