1Nitayainua macho yangu nitazame milimani. Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu unatoka kwa Yahwe, aliyezifanya mbingu na nchi.
3Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia.
4Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe.
5Yahwe ni mlinzi wako; Yahwe ni uvuli mkono wako wa kuume.
6Jua halitakudhuru wakati wa mchana, wala mwezi wakati wa usiku.
7Yahwe atakulinda na madhara yote, na ataulinda uhai wako.
8Yahwe atakulinda katika yote ufanyayo sasa na hata milele.