Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone?
2Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida?
3Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti.
4Usimuache adui yangu aseme, “Nimemshinda huyu,” ili kwamba asiweze kusema, “Nimemtawala adui yangu;” la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini.
5Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako.
6Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.