1Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
2Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia.
3Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana.
4Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.