Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 20

Luka 20:24-45

Help us?
Click on verse(s) to share them!
24“Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
25Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
26Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
30na wa pili pia.
31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
32Baadaye yule mwanamke pia akafa.
33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.'
34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.
35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.
36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.
37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake.
39“Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema.'
40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
41Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.'
44Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
45Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,

Read Luka 20Luka 20
Compare Luka 20:24-45Luka 20:24-45