Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 20:24-45 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 20:24-45 in Biblia Takatifu

24 “Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?”
25 Nao wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Yesu akawaambia, “Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Mungu vilivyo vyake Mungu.”
26 Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
27 Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu, wakasema:
28 “Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.
29 Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bila kuacha mtoto.
30 Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;
31 na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba—wote walikufa bila kuacha watoto.
32 Mwishowe akafa pia yule mwanamke.
33 Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa na wote saba.”
34 Yesu akawaambia, “Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;
35 lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.
36 Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.
37 Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
38 Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye.”
39 Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema kabisa.”
40 Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.
41 Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia
43 mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.
44 Ikiwa Daudi anamwita yeye, Bwana, basi atakuwaje mwanawe?”
45 Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,
Luka 20 in Biblia Takatifu

Luka 20:24-45 in Biblia ya Kiswahili

24 “Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
25 Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
26 Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
27 Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
28 wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
29 Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
30 na wa pili pia.
31 Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
32 Baadaye yule mwanamke pia akafa.
33 Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.'
34 Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.
35 Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.
36 Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.
37 Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
38 Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake.
39 “Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema.'
40 Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
41 Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42 Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43 mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.'
44 Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
45 Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,
Luka 20 in Biblia ya Kiswahili