Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 17

Luka 17:1-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yesu akawaambia wanafunzi wake, “mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, Lakini ole wake mtu anayeyasababisha!
2Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.
3Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe.
4Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, 'ninatubu,' msamehe!”
5Mitume wake wakamwambia Bwana, “tuongezee imani yetu.”
6Bwana akasema, “kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, 'n'goka na ukaote baharini,' nao ungewatii.
7Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, 'Njoo haraka na keti ule chakula?
8Je hatamwambia, 'Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa?
9Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa?
10Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni 'Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.'
11Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya.
12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali
13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.”
14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika.
15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu.
16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.
17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?

Read Luka 17Luka 17
Compare Luka 17:1-17Luka 17:1-17