Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 13

Luka 13:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
2Naye Yesu akawaambia, “Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo?
3Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao.
4Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
5Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao.”
6Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
7Basi, akamwambia mfanyakazi wake: Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?
8Lakini naye akamjibu: Bwana, tuuache tena mwaka huu; nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea.
9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata.”
10Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato.
11Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.”

Read Luka 13Luka 13
Compare Luka 13:1-12Luka 13:1-12