Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 13

Luka 13:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa wakataihuo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao.
2Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo?
3Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo.
4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu?
5Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia.
6Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata.
7Akamwambia mtunza bustani, 'Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani ulete uharibifu wa ardhi?
8Mtunza bustani akajibu na kusema, 'uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake.
9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate.!”'
10Sasa Yesu alikuwa akifundisha katika mojawapo ya Masinagogi wakati wa Sabato.
11Tazama, alikuwepo mama mmoja ambaye kwa miaka kumi na minane alikuwa na rohomchafu wa udhaifu, na yeye alikuwa amepinda na hana uwezo kabisa wa kusimama.
12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umewekwa huru kutoka kwenye udhaifu wako.”

Read Luka 13Luka 13
Compare Luka 13:1-12Luka 13:1-12