Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 74

Zaburi 74:1-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu, kwa nini umetukataa milele? Kwa nini hasira yako inawaka dhidi ya kondoo wa malisho yako?
2Wafikilie watu wako, ambao uliwanunua siku nyingi zilizopita, kabila ambalo wewe umelikomboa liwe urithi wako, na Milima Sayuni, mahali uishipo.
3Uje utazame uharibifu kamili, uharibifu ambao umefanywa na adui mahali patakatifu.
4Washindani wako walivamia katikati ya mahali pako maalumu; walipandisha bendera zao za vita.
5Walipakatakata kwa shoka kama katika msitu mnene.
6Walipaharibu na kuvunja sanaa zilizonakshiwa zote; walizivunja kwa shoka na nyundo.
7Walipachoma patakatifu pako; walipanajisi mahari unapoishi, wakigongagonga kwenye ardhi.
8Walisema mioyoni mwao, “Tutawaharibu wote.” Walichoma sehemu zako zote za kukutania katika nchi.
9Sisi hatuoni tena ishara; hakuna tena nabii, na hakuna yeyote miongoni mwetu ajuaye haya yatadumu kwa muda gani.
10Mpaka lini, Mungu, adui atakurushia wewe matusi? Je, atalitukana jina lako milele?

Read Zaburi 74Zaburi 74
Compare Zaburi 74:1-10Zaburi 74:1-10