1Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.”
2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako!
3Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini!
4Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe.