Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 97

Zaburi 97:1-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi.
2Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
3Moto huenda mbele zake nao huwateketeza adui zake pande zote.
4Taa yake huangaza ulimwengu; nchi huona na kutetemeka.
5Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote.
6Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake.
7Wale wote waabuduo sanamu za kuchonga wataaibishwa, wale wanao jivuna katika sanamu zisizo na maana mpigieni yeye magoti, enyi miungu wote!
8Sayuni ilisikia na kufurahi, na miji ya Yuda ilishangilia kwa sababu ya amri zako za haki, Yahwe.
9Kwa kuwa wewe, Yahwe, ndiye uliye juu sana, juu ya nchi yote. Umetukuka sana juu ya miungu yote.

Read Zaburi 97Zaburi 97
Compare Zaburi 97:1-9Zaburi 97:1-9