Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 10

Yohana 10:5-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”
6Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
7Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.
8Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.
9Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.
10Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili.
11“Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
12Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
13Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.
14Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
15kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
16Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
17“Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.
18Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
19Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”
21Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”
22Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.
23Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.
24Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi.”
25Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.
26Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.

Read Yohana 10Yohana 10
Compare Yohana 10:5-26Yohana 10:5-26