Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 10:5-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 10:5-26 in Biblia Takatifu

5 Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”
6 Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
7 Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.
8 Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.
9 Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.
10 Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili.
11 “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
12 Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
13 Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.
14 Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
16 Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
17 “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.
18 Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.”
19 Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?”
21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”
22 Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.
23 Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.
24 Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi.”
25 Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.
26 Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
Yohana 10 in Biblia Takatifu

Yohana 10:5-26 in Biblia ya Kiswahili

5 Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.”
6 Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
7 Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
8 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
9 Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
10 Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
12 Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
13 Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”
19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”
21 Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”
22 Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
25 Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
26 Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
Yohana 10 in Biblia ya Kiswahili