Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 63

Zaburi 63:1-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji.
2Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako.
3Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe.
4Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu.
5Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe,
6nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
7Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.
8Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia.
9Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi;
10watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha.

Read Zaburi 63Zaburi 63
Compare Zaburi 63:1-10Zaburi 63:1-10