Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 59

Zaburi 59:4-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Wao wanajiandaa kunikimbiza ingawa sina kosa; amka unisaidie na unitazame.
5Ewe, Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, inika uwaadhibu mataifa yote; usiwe na huruma kwa mhalifu mwovu yeyote. Selah
6Wao wanarudi jioni, wanabweka kama mbwa na kuuzungukia mji.
7Tazama, wanapiga kelele mbaya kwa midomo yao; panga ziko kwenye midomo yao, maana wanasema, “Ni nani anaye tusikia?”
8Lakini wewe, Yahwe, utawacheka; wewe huwadhihaki mataifa yote.
9Mungu, nguvu yangu, nitakuwa msikivu kwako; wewe ni mnara wangu mrefu.
10Mungu atakutana nami akiwa na uaminifu wa agano lake; Mungu atanifanya nione shauku yangu juu ya adui zangu.
11Usiwaue, hivyo watu watasahau. Uwatawanye kwa nguvu zako na uwaangushe, Bwana ngao yetu.
12Kwa ajili ya dhambi za midomo yao na maneno ya midomo yao, wakamatwe katika majivuno yao, na kwa laana na uongo ambao wao huelezea.
13Uwamalize katika gadhabu yako, uwamalize ili kwamba wasiwepo tena; wajue kuwa Mungu anatawala katika Yakobo na mwisho wa nchi. Selah
14Wakati wa jioni wao hurudi, wakibweka kama mbwa wakiuzungukia mji.
15Wanatangatanga wakitafuta chakula na wanabweka kama mbwa kama hawajatosheka.
16Lakini nitaimba kuhusu nguvu zako, na asubuhi nitaimba kuhusu upendo wako imara! maana umekuwa mnara wangu mrefu na kimbilio la usalama katika siku ya taabu.
17Kwako, nguvu yangu, nitaimba sifa; kwa kuwa Mungu ni mnara wangu mrefu, Mungu wa uaminifu wa agano.

Read Zaburi 59Zaburi 59
Compare Zaburi 59:4-17Zaburi 59:4-17