Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 52

Zaburi 52:2-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Ulimi wako hupanga uharibifu kama wembe mkali, na kufanya udanganyifu.
3Wewe unapenda uovu kuliko wema na udanganifu kuliko kuongea haki. Selah
4Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu.
5Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. Selah
6Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema,
7“Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine.”
8Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele.

Read Zaburi 52Zaburi 52
Compare Zaburi 52:2-8Zaburi 52:2-8