Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 12

Zaburi 12:2-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu.
3Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa.
4Hawa ni wale ambao wamesema, “Kwa ndimi zetu tutashinda. Wakati midomo yetu itakapo ongea, ni nani atakaye kuwa mtawala juu yetu?”
5“Kwa sababu ya vurugu zilizopo kinyume na maskini, na kwa sababu ya kuugua kwao wahitaji, Nitainuka,” asema Yahwe. “Nitawaletea usalama wanao hitaji.”
6Maneno ya Yahwe ni masafi, kama fedha iliyo safishwa katika tanuru duniani, iliyo ng'arishwa mara saba zaidi.
7Wewe ni Yahwe! Unaye watunza. Una wahifadhi wacha Mungu kutoka katika hiki kizazi cha waovu na hata milele.

Read Zaburi 12Zaburi 12
Compare Zaburi 12:2-7Zaburi 12:2-7