Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 98

Zaburi 98:1-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi.
2Yahwe ameufanya wokovu wake ujulikane; ameidhihirisha haki yake kwa mataifa yote.
3Hukumbuka uaminifu wa agano lake na uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia itauona ushindi wa Mungu wetu.
4Mshangilieni Yahwe, nchi yote; pazeni sauti kwa wimbo, imbeni kwa furaha, na imbeni sifa.
5Mwimbieni Yahwe sifa kwa kinubi, kwa kinubi na wimbo wenye muiki wa kupendeza.
6Kwa panda na sauti ya baragumu, fanyeni kelele za shangwe mbele ya Mfalme, Yahwe.
7Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake!
8Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha.
9Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.

Read Zaburi 98Zaburi 98
Compare Zaburi 98:1-9Zaburi 98:1-9