Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 94

Zaburi 94:4-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Wanamwaga maneno yao ya kiburi; wote watendao uovu wanajivuna.
5Wanawaangamiza watu wako, Yahwe; wanalitesa taifa ambao ni milki yako.
6Wanamuua mjane na mgeni aishiye nchini mwao, na wanamuua yatima.
7Nao husema, “Yahwe hawezi kuona, Mungu wa Yakobo hayagundui haya.”
8Tambueni, ninyi watu wajinga! Enyi wapumbavu, mtajifunza lini?
9Yeye aliye liumba sikio, hasikii? Yeye aliye litengeneza jicho, haoni?
10Yeye awaadhibuye mataifa, hayuko sahihi? Yeye ndiye ampaye maarifa mwanadamu.
11Yahwe anayajua mawazo ya wanadamu, kuwa ni mvuke.
12Amebarikiwa yule ambaye umuongozaye, Yahwe, yule ambaye wewe humfundisha kutoka katika sheria yako.
13Wewe humpa pumziko wakati wa shida mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa kwa ajili ya waovu.
14Maana Yahwe hatawaacha watu wake wala kutelekeza warithi wake.

Read Zaburi 94Zaburi 94
Compare Zaburi 94:4-14Zaburi 94:4-14