9Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa.
10Wewe umeyainua mapembe yangu kama mapembe ya Nyati wa porini; nimepakwa mafuta safi.
11Macho yangu yameona kuanguka kwa adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya maadui zangu waovu.
12Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni.
13Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe; wakistawi katika nyua za Mungu wetu.
14Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya,
15kutangaza kuwa Yahwe ni wa haki. Yeye ni mwamba wangu, na hakuna udhalimu ndani yake.