1Sikia, Ee Yahwe, na unijibu, kwa kuwa ni maskini na mnyonge.
2Unilinde, maana mimi ni mwaminifu; Mungu wangu, umuokoe mtumishi wako anayekuamini.
3Unihurumie, Bwana, maana ninakulilia wewe mchana kutwa.
4Umfurahishe mtumishi wako, maana ni kwako, Bwana, ninaomba.
5Wewe, Bwana, ni mwema, na uko tayari kusamehe, na huonesha huruma kubwa kwa wale wanao kulilia wewe.
6Yahwe, sikiliza maombi yangu; sikia sauti ya ombi langu.
7Katika siku ya shida ninakuita wewe, kwa maana utanijibu.