Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 82

Zaburi 82:1-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.
2Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah
3Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.
4Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.
5Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.
6Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.
7Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”
8Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.

Read Zaburi 82Zaburi 82
Compare Zaburi 82:1-8Zaburi 82:1-8