1Nitampazia Mungu sauti yangu, nitamuita Mungu kwa sauti yangu, na Mungu wangu atanisikia.
2Katika siku ya taabu nilimtafuta Bwana; usiku niliinua mikono yangu, nayo haikuchoka. Moyo wangu ulikataa kufarijiwa.
3Ningali nikiugua nilielekeza mawazo yangu kwa Mungu. Nilimfikiria Mungu nilipokuwa dhaifu. Selah
4Uliyafanya macho yangu yasisinzie; nilisumbuka sana kuongea.
5Nilifikiri kuhusu siku za kale, kuhusu mambo yaliyopita muda mrefu.
6Wakati wa usiku niliukumbuka wimbo niliouimba mara moja. Nilifikiria kwa makini na kujaribu kuelewa kile kilichokuwa kimetokea.
7Je, Mungu atanikataa milele? Je, hatanionesha tena huruma?
8Je, uaminifu wa agano lake ulikuwa umetoweka milele? Je, ahadi yake imeshindwa milele?
9Je, Mungu amesahau kuwa mwenye neema? Je, hasira yake imeifunga huruma yake? Selah
10Nilisema, “Hii ni huzuni yangu: mabadiliko ya mkono wa kuume wa Aliye Juu dhidi yetu.”
11Lakini nitayakumbuka matendo yako, Yahwe; nitafikiri kuhusu matendo yako makuu yaliyopita.
12Nitayatafakari matendo yako yote nami nitayaishi.
13Njia yako, Mungu, ni takatifu; ni mungu gani wa kulinganishwa na Mungu wetu aliye mkuu?
14Wewe ni Mungu utendaye maajabu; wewe umeonesha nguvu zako kati ya mataifa.
15Uliwapa watu wako ushindi kwa uweza wako mkuu - ukoo wa Yakobo na Yusufu. Selah
16Maji yalikuona wewe, Mungu; maji yalikuona wewe, nayo yakaogopa; vina vya maji vilitetemeka.
17Mawingu yalitiririsha maji chini; anga zito lilitoa sauti; mishale yako ilipita kati.