Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 77:1-17 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 77:1-17 in Biblia ya Kiswahili

1 Nitampazia Mungu sauti yangu, nitamuita Mungu kwa sauti yangu, na Mungu wangu atanisikia.
2 Katika siku ya taabu nilimtafuta Bwana; usiku niliinua mikono yangu, nayo haikuchoka. Moyo wangu ulikataa kufarijiwa.
3 Ningali nikiugua nilielekeza mawazo yangu kwa Mungu. Nilimfikiria Mungu nilipokuwa dhaifu. Selah
4 Uliyafanya macho yangu yasisinzie; nilisumbuka sana kuongea.
5 Nilifikiri kuhusu siku za kale, kuhusu mambo yaliyopita muda mrefu.
6 Wakati wa usiku niliukumbuka wimbo niliouimba mara moja. Nilifikiria kwa makini na kujaribu kuelewa kile kilichokuwa kimetokea.
7 Je, Mungu atanikataa milele? Je, hatanionesha tena huruma?
8 Je, uaminifu wa agano lake ulikuwa umetoweka milele? Je, ahadi yake imeshindwa milele?
9 Je, Mungu amesahau kuwa mwenye neema? Je, hasira yake imeifunga huruma yake? Selah
10 Nilisema, “Hii ni huzuni yangu: mabadiliko ya mkono wa kuume wa Aliye Juu dhidi yetu.”
11 Lakini nitayakumbuka matendo yako, Yahwe; nitafikiri kuhusu matendo yako makuu yaliyopita.
12 Nitayatafakari matendo yako yote nami nitayaishi.
13 Njia yako, Mungu, ni takatifu; ni mungu gani wa kulinganishwa na Mungu wetu aliye mkuu?
14 Wewe ni Mungu utendaye maajabu; wewe umeonesha nguvu zako kati ya mataifa.
15 Uliwapa watu wako ushindi kwa uweza wako mkuu - ukoo wa Yakobo na Yusufu. Selah
16 Maji yalikuona wewe, Mungu; maji yalikuona wewe, nayo yakaogopa; vina vya maji vilitetemeka.
17 Mawingu yalitiririsha maji chini; anga zito lilitoa sauti; mishale yako ilipita kati.
Zaburi 77 in Biblia ya Kiswahili