Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 37

Zaburi 37:5-36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Umkabidhi njia zako Yahwe; uamini katika yeye, naye atatenda kwa niaba yako.
6Yeye ataidhihilisha haki yako kama mchana na usafi wako kama mwangaza wa mchana.
7Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.
8Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
9Watendao maovu watafutiliwa mbali, bali wale wamngojao Yahwe watairithi nchi.
10Katika muda mfupi mtu mwovu atatoweka; wewe utatazama mahali pake, wala hautamuona.
11Lakini wapole watairithi nchi nao watafurahia katika mafanikio makubwa.
12Mtu mwovu hupanga njama kinyume na mwenye haki na kumsagia meno.
13Bwana humcheka, kwa maana anaona siku yake inakuja.
14Waovu wametoa nje panga zao na wametayarisha pinde zao ili kuwaangamiza wanyonge na wahitaji, na kuwaua wenye haki.
15Panga zao zitawaua wenyewe, na pinde zao zitavunjika.
16Ni bora kuwa mwenye haki maskini kuliko tajiri mwenye mali nyingi.
17Kwa maana mikono ya watu waovu itavunjika, bali Yahwe huwasaidia watu wenye haki.
18Yahwe huwalinda watu wasio na lawama siku hadi siku, na urithi wao utakuwa wa milele.
19Hawata aibika siku mbaya zijapo. Wakati wa njaa ufikapo wao watakuwa na chakula cha kutosha.
20Bali waovu wataangamia. Maadui wa Yahwe watakuwa kama vile utukufu wa malisho; watamalizwa na kupotezwa katika moshi.
21Mtu mwovu hukopa lakini halipi, bali mtu mwenye haki ni mkarimu na hutoa.
22Wale walio barikiwa na Mungu watairithi nchi; wale aliowalaani watafutiliwa mbali.
23Hatua za mwanadamu zinaimarishwa na Yahwe, mtu ambaye njia zake zinakubalika machoni pa Mungu.
24Ajapojikwaa, hataanguka chini, kwa kuwa Yahwe anamshikilia kwa mkono wake.
25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; sijawahi kumuona mtu mwenye haki ametelekezwa wala watoto wake kuombaomba mkate.
26Wakati wote yeye ni mkarimu na hukopesha, nao watoto wake hufanyika baraka.
27Acha uovu na ufanye yaliyo mema; ndipo utakapokuwa salama milele.
28Kwa maana Yahwe hupenda haki naye hawaachi wafuasi waaminifu. Wao hutunzwa milele, lakini uzao wa waovu utafutiliwa mabli.
29Wenye haki watairithi nchi na kuaa huko milele.
30Mdomo wa mwenye haki huongea hekima na huongeza haki.
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; miguu yake haitelezi.
32Mtu mwovu humvizia mwenye haki na kutafuta kumuua.
33Yahwe hatamuacha yeye kwenye mkono wa mtu mwovu wala kumlaumu atakapohukumiwa.
34Umngoje Yahwe na uishike njia yake, naye atakuinua uimiliki nchi. Atakapo waondosha waovu wewe utaona.
35Nimewaona waovu na mtu wa kutisha akienea kama mti wa kijani katika udongo wa asili.
36Lakini nilipopita tana mara nyingine, hakuwepo pale. nilimtafuta, lakini sikumpata.

Read Zaburi 37Zaburi 37
Compare Zaburi 37:5-36Zaburi 37:5-36