Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 22

Zaburi 22:1-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali na wokovu wangu na mbali na maneno yangu yenye uchungu?
2Mungu wangu, ninalia mchana kutwa, lakini haunijibu, na wakati wa usiku sinyamazi!
3Bado wewe ni mtakatifu; wewe umekaa kama mfalme pamoja na sifa za Israeli.
4Mababu zetu walikuamini wewe, na wewe uliwaokoa wao.
5Walikulilia wewe nao waka okolewa. Wao walikuamini wewe na hawakuvunjwa moyo.
6Bali mimi ni funza na sio mtu, nisiye faa kwa ubinadamu na hudharauliwa na watu.
7Wale wote wanionao hunisuta; hunidhihaki; hunitikisia vichwa vyao.
8Wao husema, “Yeye anamwamini Yahwe; mwache Yahwe amuokoe. Mwache amuokoe yeye, kwa kuwa yeye anampendeza sana Yeye.”
9Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.

Read Zaburi 22Zaburi 22
Compare Zaburi 22:1-9Zaburi 22:1-9