1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane!
2Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa.
3Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki.
4Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao.
5Jua liko kama mfano wa bwana harusi akitokea chumbani kwake na kama mtu shujaa ambaye hushangila pale anapokimbia mbio zake.
6Jua huchomoza kutokea upeo wa macho na likikatisha winguni kwenda jingine; hakuna chochote kinacho epuka joto lake.
7Sheria ya Yahwe ni kamilifu, huokoa roho; ushuhuda wa Yahwe ni wa kuaminika, ukifanya hekima nyepesi.
8Maelekezo ya Yahwe ni ya hakika, yakiufanya moyo kuwa na furaha; amri ya Yahwe ni safi, ikileta mwanga kwenye macho yetu.