1Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu.
2Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao.
3Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi.
4Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu.
5Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao.
6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao
7kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu.
8Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa.