1Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe, ninyi mlio katika mbingu; msifuni yeye, ninyi mlio juu.
2Msifuni yeye, enyi malaika wake wote; msifuni yeye, majeshi ya malaika wake wote.
3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi; msifuni yeye, nyota zote zing'aazo.
4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu zaidi na maji yaliyo juu ya anga.
5Na vilisifu jina la Yahwe, maana aliamuru, navyo vikaumbwa.
6Pia ameviimrisha milele na milele; naye alitoa amri ambayo haitabadilika.
7Msifuni yeye kutoka nchi, ninyi viumbe wa baharini na viumbe vyote katika kina cha bahari,
8moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba ukitimiza neno lake.
9Msifuni yeye, enyi milima na vilima, miti ya matunda na mierezi yote,