1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe, ninyi mlio katika mbingu; msifuni yeye, ninyi mlio juu.
2 Msifuni yeye, enyi malaika wake wote; msifuni yeye, majeshi ya malaika wake wote.
3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi; msifuni yeye, nyota zote zing'aazo.
4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu zaidi na maji yaliyo juu ya anga.
5 Na vilisifu jina la Yahwe, maana aliamuru, navyo vikaumbwa.
6 Pia ameviimrisha milele na milele; naye alitoa amri ambayo haitabadilika.
7 Msifuni yeye kutoka nchi, ninyi viumbe wa baharini na viumbe vyote katika kina cha bahari,
8 moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba ukitimiza neno lake.
9 Msifuni yeye, enyi milima na vilima, miti ya matunda na mierezi yote,