Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 142

Zaburi 142:2-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Namwaga malalamiko yangu mbele zake; ninamwambia shida zangu.
3Roho yangu inapokuwa dhaifu ndani yangu, wewe unajua mapito yangu. Kwenye njia niipitayo wamenifichia mtego.
4Natazama kulia kwangu na sioni yeyote anayenijali. Sina pa kukimbilia; hakuna anayejali kuhusu uhai wangu.
5Nilikuita wewe, Yahwe; nikasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.
6Sikia kuita kwangu, maana nimeshushwa chini sana; uniokoe dhidi ya watesi wangu, maana wana nguvu kuliko mimi.
7Uitoe nafsi yangu kifungoni ili niweze kulishukuru jina lako. Wenye haki watakusanyika karibu nami kwa sababu umekuwa mwema kwangu.”

Read Zaburi 142Zaburi 142
Compare Zaburi 142:2-7Zaburi 142:2-7