Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 132

Zaburi 132:2-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Kumbuka ndiye aliye mwapia Yahwe, aliweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.
3Alisema, sitaingia nyumbani mwangu wala sitaenda kitandani mwangu,
4sitayapa macho yangu usingizi wala kope zangu kupumzika
5mpaka nitakapopata mahali kwa ajili ya Yahwe, na maskani kwa ajili ya Shujaa wa Yakobo.”
6Tazama tulisikia kuhusu hilo katika Efrata; tuliipata katika konde la Yearimu.
7Tutaingia katika maskani ya Mungu; tutasujudu miguuni pake.
8Inuka, Ee Yahwe, uje mahali pako pa kupumzika, wewe na sanduku la nguvu zako!
9Makuhani wako na wavikwe uadilifu; waaminifu wako washangilie.
10Kwa ajili ya mtumishi wako Daudi, usimuache mfalme wako uliye mpaka mafuta.
11Yahwe alimwapia Daudi kiapo cha uhakika, kiapo cha uhakika ambacho hatakivunja: “Nitamuweka mmoja wa wazawa wako kwenye kiti chako cha enzi.

Read Zaburi 132Zaburi 132
Compare Zaburi 132:2-11Zaburi 132:2-11