Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 96

Zaburi 96:5-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, bali ni Yahwe aliye zifanya mbingu.
6Heshima na adhama ziko mbele zake. Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7Mpeni Yahwe sifa, enyi ukoo wa watu, mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu.
8Mpeni Yahwe utukufu ambao unastahili jina lake. Leteni matoleo na muingie nyuani mwake.
9Mpigieni magoti Yahwe mkiwa mmevaa mavazi ambayo yanaheshimu utakatifu wake. Nchi yote tetemekeni mbele zake.
10Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala.” Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
11Mbingu na zifurahi, na nchi ishangilie; bahari na ivume na vyote viijazavyo vipige kelele kwa shangwe.

Read Zaburi 96Zaburi 96
Compare Zaburi 96:5-11Zaburi 96:5-11