Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 57

Zaburi 57:1-4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
2Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu.
3Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. Selah Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake.
4Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga.

Read Zaburi 57Zaburi 57
Compare Zaburi 57:1-4Zaburi 57:1-4