12Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi; maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.
13Je! sitakula nyama ya ngombe na kunywa damu ya mbuzi?
14Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu.
15Mniite katika siku ya shida; nami nitawaokoa
16Lakini kwa waovu Mungu anasema, “Inawahusu nini kuitangaza hali yangu, kwamba ninyi mmeliweka agano langu mdomoni mwenu,
17wakati ninyi mnayachukia maelekezo na mnayatupa maneno yangu?
18Mumuanapo mwizi, ninyi hukubaliana naye; ninyi na mnashirikiana na wale wafanyao uasherati.
19Mwautoa mdomo wenu kwa mabaya, huelezea udanganyifu.
20Mnakaa na kuongea dhidi ya ndugu yenu; na kukashfu mwana wa mama yenu.
21Mmefanya mambo haya, lakini nimekaa kimya, hivyo mlidhani kuwa ni mtu flani nilliye kama ninyi mlivyo. Lakini nitawakaripia ninyi na kuwafunua, mbele ya macho yenu, mambo yote miliyofanya.
22Mlitilie maanani hili, ninyi mnao msahau Mungu, vinginevyo nitawakata ninyi vipande vipande, na hatakuwepo yeyote wakuja kuwasaidia!
23Yule atoaye sadaka ya shukurani hunitukuza, na yeyote apangaye njia zake katika namna iliyo sahihi nitamuonesha wokovu wa Mungu.”