8Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah
9Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.
10Umetufanya kuwakimbia maadui zetu; na wale watuchukiao huchukua vitu vyetu vya thamani kwa ajili yao wenyewe.
11Umetufanya kama kondoo aliyeandaliwa kwa ajili ya chakula na umetutawanya kati ya mataifa.
12Wewe unawauza watu wako bure; kwa kufanya hivyo haukupata faida.
13Wewe umetufanya kukemewa na majirani zetu, kuchekwa, na kudhihakiwa na wale wanao tuzunguka.
14Umetufaya kituko kati ya mataifa,...