Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 21

Zaburi 21:8-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Mkono wako utawakamata adui zangu wote wote; mkono wako wa kuume utawakamata wale wote wanao kuchukia.
9Wakati wa hasira yako, wewe utawachoma kama katika tanuru la moto. Yahwe atawamaliza wao katika hasira yake, na moto utawateketeza upesi wao.
10Wewe utawaangamiza watoto wao duniani na ukoo wao kutoka katika mrorongo wa wanadamu.
11Kwa kuwa walikusudia kukufanyia mambo maovu wewe; wao walitunga njama ambayo kwayo hawawezi kufanikiwa!
12Kwa kuwa wewe utawarudisha nyuma; wewe utafyatua upinde wako mbele yao.
13Uninuliwe, Yahwe, katika uweza wako; tutaimba na kusifu nguvu zako.

Read Zaburi 21Zaburi 21
Compare Zaburi 21:8-13Zaburi 21:8-13