9Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari,
10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika.
11Kama nikisema, “Hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo itakuwa usiku,”
12Hata giza lisingweza kuwa giza kwako. Usiku ungeng'aa kama mchana, maana giza na nuru kwako vinafanana.
13Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu.
14Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana.
15Mifupa yangu haikusitirika kwako nilipoumbwa kwa siri, nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi.
16Uliniona ndani ya tumbo; siku zote zilizo pangwa kwangu ziliandikwa kitabuni mwako hata kabla ya siku ya kwanza kutokea.
17Ni jinsi gani mawazo yako ni ya thamani kwangu, Mungu! Njinsi ilivyo kubwa jumla zake!
18Kama nikijaribu kuyahesabu ni mengi kuliko mchanga. Niamkapo bado niko na wewe.
19Ee Mungu, kama ungewaua waovu; ondokeni kwangu enyi watu wenye vurugu.
20Wanakuasi wewe na kutenda udanganyifu; adui zako wananena uongo.
21Je, siwachukii hao, wale wakuchukiao Yahwe? Je, siwadharau wale wanao inuka dhidi yako?
22Nawachukia kabisa; wamekuwa adui zangu.