Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 17

Yohana 17:13-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
14Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
15Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
16Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
17Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
18Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
19Kwa ajili yao mimi mwenyewe ninajitoa kwako ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli.
20Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao
21ili kwamba wao nao wawe na umoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
22Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa na umoja, kama vile sisi tulivyo umoja -
23Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.
24Baba, kile ulichonipa mimi - Natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

Read Yohana 17Yohana 17
Compare Yohana 17:13-24Yohana 17:13-24