Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 17:13-24 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 17:13-24 in Biblia Takatifu

13 Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.
14 Mimi nimewapa neno lako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
15 Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
17 Waweke wakfu kwa ukweli; neno lako ni ukweli.
18 Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
19 na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli.
20 “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao.
21 Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
22 Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;
23 mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
24 “Baba! Nataka wao ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Yohana 17 in Biblia Takatifu

Yohana 17:13-24 in Biblia ya Kiswahili

13 Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
14 Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
15 Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
17 Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
19 Kwa ajili yao mimi mwenyewe ninajitoa kwako ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli.
20 Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao
21 ili kwamba wao nao wawe na umoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
22 Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa na umoja, kama vile sisi tulivyo umoja -
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.
24 Baba, kile ulichonipa mimi - Natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.
Yohana 17 in Biblia ya Kiswahili