Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 17

Yohana 17:13-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.
14Mimi nimewapa neno lako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
15Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.
16Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
17Waweke wakfu kwa ukweli; neno lako ni ukweli.
18Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
19na kwa ajili yao mimi mwenyewe najiweka wakfu ili nao pia wafanywe wakfu katika ukweli.
20“Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao.
21Naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba! Naomba wawe ndani yetu kama vile wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Naomba wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.
22Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;
23mimi niwe ndani yao, nawe uwe ndani yangu; naomba wakamilishwe na kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kujua kwamba wewe ulinituma, na kwamba unawapenda wao kama unavyonipenda mimi.
24“Baba! Nataka wao ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili wauone utukufu wangu ulionipa; kwa kuwa ulinipenda kabla ya kuumbwa ulimwengu.

Read Yohana 17Yohana 17
Compare Yohana 17:13-24Yohana 17:13-24